BREAKING

Tuesday, 10 March 2020

BRAND KENYA YATUA JIJINI DAR ES SALAAM .....



The High Commissioner of the Republic of Kenya in the United Republic of Tanzania Amb. Dan Kazungu on Monday received a high- level trade mission from Kenya’s Export and Branding Agency, Brand.KE. The trade delegation was led by the Chief Executive Officer Mr. Peter Biwott. The trade mission is in Dar es salaam to hold consultations with key Tanzanian trade and investment promotion organisations in a bid to promote and enhance bilateral trade between Kenya and Tanzania. These include Tanzania Trade and Development Authority (TANTRADE), Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA) and Tanzania Private Sector Foundation (TPSF).
Kenya’s High Commissioner Amb. Dan Kazungu with Mr. Peter Biwott, CEO of Brand.KE holding discussions during the latter’s visit at the Kenya High Commission on Monday9th March 2020
While welcoming the delegation, Amb. Dan Kazungu mentioned that 48 percent of intra East African Community (EAC) trade occurs between Kenya and Tanzania which is an indication of the interdependence that exists between the two countries. He added that there is need for both Kenyans and Tanzanians to cooperate even more for shared prosperity.
On his part, Mr. Biwott said that it was a high time that Kenyans and Tanzanians focused more on cross border trade that would boost each other’s economies more as opposed to seeking foreign markets whose returns were much lower. Mr. Biwott also noted that Kenya and Tanzania are unique countries with vast opportunities ranging from agriculture, infrastructure, services, mining, logistics and the blue economy. In addition, there are opportunities for Kenyan companies in the financial service sector. These opportunities can be seized through partnerships with Tanzanian companies.
Brand.KE is a State Corporation established under the State Corporations Act Cap 446 through Legal Notice No.110 of August 9th, 2019 after the merger of the Export Promotion Council and Brand Kenya Board. The Brand.KE mandate is to implement export promotion and nation branding initiatives and policies to promote Kenya’s export of goods and services.
Brand.KE CEO Mr. Peter Biwott signing the visitor’s book at the Kenya High Commission. With him is Kenya’s High Commissioner Amb. Dan Kazungu
Kenyan companies, through Brand.KE, will participate in the 44th Dar es Salaam International Trade Fair (DITF) slated for June and July 2020. Brand.KE has reserved a substantive number of booths for this years’ event that promises Kenyan high-level participation and a showcase of how trade and investment is undertaken in the East African region and beyond.
The DITF presents Kenyan companies to invest in Tanzania as well as export their goods and services while at the same time, offering opportunities to the Tanzanian private sector in so far as market and product diversification is concerned. Thus, participation in the Trade Fair will enhance trade, investment and tourism with a view to promote accelerated economic growth and development between the two countries and East Africa as well as the African continent.
Brand.KE in conjunction with the Kenya High Commission Dar es Salaam will organize a high-level business forum, an elaborate diaspora engagement and high-level participation at the Dar es Salaam International Trade Fair (DITF) between March and July 2020. The trade mission will focus its activities in four regions in its bid to boost the distribution channel of Kenyan goods in Tanzania. These include: - Mwanza (Mwanza region), Arusha and Moshi (Kilimanjaro region), Dar es Salaam (Dar es Salaam and Coast regions) and Mbeya (Southern region).
Brand.KE are also planning a second visit that will focus on developing an elaborate distribution channel for Kenyan goods in Dodoma (Central Tanzania) and Zanzibar in a carefully conceived and deliberate strategy to promote Kenyan exports in the United Republic of Tanzania.
Amb. Dan Kazungu receives a gift from Mr. Peter Biwott, CEO of Brand.KE at the Kenya High Commission on Monday 9th March 2020
The Kenya High Commission in Dar es Salaam is upbeat that these efforts will improve the trade performance that stands at Kshs 33.5 billion in January 2020, up from Kshs 28 billion in 2018.

ISUPILO HAKUNA ARDHI YA KUGAWAKWA WANANCHI,MIPAKA YA GEREZA ILINDWE.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikongosi wilaya ya Mufindi

NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.
 
MKUU wa magereza la Isupilo Benjamin Kabisa wamejipanga kulinda ardhi ya magereza kwa kuwa  Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amegiza kuwa magereza yote kuanza kujitegemea kwa kuzalisha chakula kupitia wafungwa.


Hoja hiyo imekuja mara baada ya wananchi wa kijiji cha Ikongosi wilaya ya Mufindi la kuomba ardhi ya kulima katika eneo la jeshi la magereza kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi wakati wa ziara ya Iringa mpya awamu ya pili.


Benjamin alisema kuwa eneo la gereza la Isupilo mipaka yake inajulikana na ipo kisheria nay eye hawezi kugawa eneo hilo hadi pale mamla za juu za serikali zitakavyo amua kwa kuwa kila kitu kipo kimaandishi.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alikataa ombi hilo kwa wananchi wa kijiji cha Ikongosi  wakati wa mkutano wa kupokea kero za wananchi wa wilaya ya Mufindi.


Alisema kuwa ardhi ya magereza ni kwa ajili ya matumizi ya magereza kuzalisha chakula kwa ajili ya wafungwa.

hata hivyo Hapi alisema kuwa sio kila ombi la wananchi anatakiwa kuwatekelezea kwani kimsingi ardhi ya magereza ni maalum kwa ajili ya utaratibu wa serikali kuhifadhi ardhi yake kwa ajili ya matumizi yake ya baadae.

"Serikali ina kawaida ya kuwekeza benki ya Ardhi kwa ajili ya matumizi ya kijamii ikija kutokea wananchi wameongezeka na serikali inahitaji kujenga kituo cha afya ama shule benki yake ya ardhi ni kwenye ardhi hiyo iliyowekezwa kwenye taasisi zake kama magereza,jeshi la kujenga Taifa na maeneo mengine"

Aidha alisema iwapo wananchi wanahitaji eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule wanaweza kukaa chini na Magereza ili kupewa eneo Ila sio kwa ajili ya kilimo .

Alisema kimsingi shule ni mali ya serikali na magereza ipo chini ya serikali hivyo wanaweza kupewa eneo la ujenzi na kuwekewa mipaka.

"Ila niwaeleze wazi wananchi kuwa sio kila ombi mnaloomba mnaweza kusikilizwa maombi mengine hayawezekani kama hili la kuomba ardhi ya magereza kwa ajili ya kulima  watu binafsi"


Hata hivyo Hapi aliagiza magereza kutumia wafungwa kuendeleza ardhi hiyo kwa kilimo Kama Rais Dkt John Magufuli alivyoagiza kwa magereza zote nchini kutumia wafungwa kuzalisha chakula Chao wenyewe.

TARURA SITISHENI UJENZI WA BARABARA ZA VUMBI HADI MVUA ZITAKAPO SIMAMA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akizungumza kwenye ziara ya Iringa mpya awamu ya pili alipokuwa anakagua ujenzi wa barabara yaKinyanambo, Pareto,Chumi,Lutherani na Mwamkoa Mbagala iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga akiwataka wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) kusitisha ujenzi wa barabara hizo kwa kuwa ujenzi huo hauna tija kwa wananchi
 Baadhi ya uharibifu unaondelea kwenye maeneo ambayo ujenzi wa barabara unaendelea hivi sasa kwenye maeneo ya Mji wa Mafinaga Mji.
 Baadhi ya uharibifu unaondelea kwenye maeneo ambayo ujenzi wa barabara unaendelea hivi sasa kwenye maeneo ya Mji wa Mafinaga Mji

NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.

SERIKALI ya mkoa wa Iringa imewataka wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) kusitisha ujenzi wa barabara za vumbi zinazoendelea kujengwa na wakandarasi mbalimbali kutokana mvua kubwa zinazoendelea hivi sasa.

Akizungumza kwenye ziara ya Iringa mpya awamu ya pili alipokuwa anakagua ujenzi wa barabara yaKinyanambo, Pareto,Chumi,Lutherani na Mwamkoa Mbagala iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga,mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi aliwataka wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) kusitisha ujenzi wa barabara hizo kwa kuwa ujenzi huo hauna tija kwa wananchi.

Kipindi hiki mvua zinanyesha kwa wingi kila kona na zimekuwa zikiharibu miundombinu katika maeneo mengi katika mkoa huu wa Iringa,hivyo kutokana na hali hiyo natangaza kusitisha ujenzi wa barabara hizo hadi pale mvua zitakapo isha.

Hapi aliwataka viongozi wa TARURA kuhakikisha wanawasimamia vilivyo wakandarasi wote wanajenga barabara hizo ili zijengwe katika ubora unatakiwa kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

“Hakikisheni mnawasimamia vilivyo wakandarasi hao kwa kuwa fedha zinazotumika ni kodi za wananchi hao ambao mnawaona hapa,hivyo lazima thamani ya fedha hizo ionekane kwa wananchi hawa” alisema Hapi

Hapi aliwataka TARURA kuongeza kasi ya ujenzi wa mitandao ya barabara za lami katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga na ujenzi wa taa za barabarani ili Halmashauri ya Mji wa Mafinga kuwa Manispaa na hatimaye mkoa wa Iringa kuwa Jiji.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliamu aliwataka TARURA  kujenga mitaro yenye ubora unaotakiwa ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa inamudu maji yote yanayopita na kuzilinda barabara zisiaharibike haraka na zidumu kwa muda mrefu.

“Barabara zetu nyingi za wilaya hii zinaharibika kutokana na kutokuwa na mitaro iliyobora inayohimili maji mengi na ndio maana barabara zinaharibika kila uchwao hizi ni bora kuweni wakali kwa wakandarasi wanaopewa tenda za mitaro kwenye barabara husika” alisema Wiliam

Akijibia hoja za mkuu wa mkoa,mwananchi Inocent Mahanga na mkuu wa wilaya ya Mufindi,meneja wa TARURA Mafinga Tc Injinia Simoni Ngagani alisema kuwa watahakikisha barabara zinajengwa kwenye ubora unatakiwa kulingana na thamani ya fedha za mradi husika.

Tutahakikisha ujenzi wa Mifereji na barabara zinajengwa kwa viwango stahili ili kutumia vilizuri kodi za wananchi


 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube