skip to main |
skip to sidebar
Leo ni Nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi ambapo Yanga watawakabili Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Aman Zanzibar.
Mchezo huo utapigwa jioni ya leo ambapo watani wao wa jadi Simba watashuka Dimbani kumenyana na Mabingwa wa kombe hilo Azam FC na iwapo timu hizo zenye upinzani mkubwa zitakutana fainali basi kwa msimu huuu watakuwa wamekutana mara mbili na huenda wakakutana mara tatu ......
KHLEFFIN Hamdoun, kiungo mshambuliaji aliyekuwa akiitumikia Mlandege ya Zanzibar amemalizana na Azam FC kwa kusaini kandarasi ya miaka minne.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba alivutiwa na uwezo wa nyota huyo baada ya kumuona kwenye mchezo wa robo fainali wa Kombe la Mapinduzi ambapo Azam FC ilishinda kwa bao 1-0.
Katika moja ya mchezo uliochezwa katika michuano ya mapinduzi kati ya Mlandege na Azam Mtangazaji wa Azam Sports Ahmed Ally alimhoji juu ya kuijunga na Azam Khleffin Hamdoun alikana lakini sasa mambo hadharani.
Huu ni usajili wa kwanza kwa Azam FC msimu huu kwenye dirisha dogo lililofunguliwa mwezi, Desemba 15, 2019.