BREAKING

Tuesday, 26 February 2019

BENKI YA STANDARD CHARTERED KUWEZESHA HUDUMA ZA KIBENKI ZAIDI YA 70 KIDIGITALI

 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dk. Bernard Kibesse,akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa programu ya Standard Chartered Tanzania Digital App.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya uzi nduzi wa programu ya Standard Chartered Tanzania Digital App uliofanyika katika hoteli ya Hyatt.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bernard Kibesse (Kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani,Balozi wa Programu mpya ilizozinduliwa,Vanessa Mdee na Mkuu wa huduma za kibenki wa wateja wadogo wa Benki hiyo, Ajmair Riaz ,wakionyesha miondoko ya UNSTOPABLE wakati wa hafla ya uzinduzi

REPSSI YAENDELEA NA KAMPENI KUTOKOMEZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimbaMkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimba
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala 

Mwandishi wetu, Pwani.

Shirika linalojihusisha na masuala ya kijamii na kisaikolojia kwa watoto (REPPSI) limeendelea kufanya kampeni ya kutokomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni mkoani Pwani.

Kampeni hiyo inafanyika ili kuhakikisha watoto wa kike wanatimiza ndoto zao za kielimu ili kushiriki katika mkakati wa Serikali wa Tanzania ya viwanda.

Akizungumza na wakazi wa Kibiti Mkoani Pwani, Mkurugenzi Mkazi wa REPSI Tanzania, Edwick Mapalala alisema tatizo la mimba na ndoa za utotoni bado kubwa na kwamba linahitaji jitihada za pamoja kupambana nalo.

“Mfano ni hizi kampeni za kutoa elimu na kuihamasisha jamii kumthamini mtoto wa kike zinasaidia kwa hiyo kama tutaendelea nazo jamii itaelewa, watoto watatimiza ndoto zao,” alisema.

Mapalala alisema katika kampeni hizo wanazoshirikiana na Shirika la Pasada linalojihusisha na masuala ya Ukimwi chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Pwani, vijana hasa madereva bodaboda wamefikishiwa elimu kuhusu thamani ya mtoto wa kike.

Baadhi ya viongozi wa vijiji na kata walikiri kuwa ndoa za utotoni ni changamoto kubwa lakini wanaendelea kupambana nayo.

Mratibu wa Elimu Kata ya Salala, Wilayani Kibiti Erasmus Assenga alisema kwa mwaka huu tu wanafunzi wawili wa Sekondari katika kata hiyo wameacha masomo kwa mimba.

“Kwa hiyo kampeni hii ni muhimu kwa sababu watoto wa kike wenyewe wanafikishiwa elimu, jamii hasa wanaume wanaelezwa na wanajua umuhimu wa kuwathamini,” alisisitiza.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Pasada Ester Mbwana alisema anaamini kuwa baada ya kampeni hizo kutakuwa na mafanikio makubwa kwa sababu, jamii inaelewa na imekubali kusaidia katika ulinzi wa mtoto.

Wednesday, 6 February 2019

TRC YAWAPA SHAVU WASANII KUTEMBELEA MRADI WA RELI YA KISASA YA STARDARD GAUGE

Kiongozi wa Wasanii, Steve Nyerere akuongea na wanahabari kuwaelezea madhumuni ya Safari ya wasanii wote katika wote Februari 7, 2019 kutembelea mradi wa Reli ya Kisasa ya reli ya Kisasa ya Standard Gauge inayoanzia Dar es Salaam na kuelekea Morogoro. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Kaimu Mtendaji Mkuu wa shirika la reli nchini (TRC) Jamila Mbarouk (kulia) akiongea na wanahabari jinsi walivyoweza kudhamini wasanii hao kutembelea Mradi wa mradi wa Reli ya Kisasa ya reli ya kisasa ya Standard Gauge inayoanzia Dar es Salaam na kuelekea Morogoro ambapo amesema kuwa wametoa nafasi hiyo ili wasanii wakienda, warudi na watoe ushuhuda wa kweli kwa wananchi maana wao ni kioo cha jamii.
Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka ambaye ni mwakilishi wa wamiliki na wasanii wa bendi za muziki wa Dance akitoa machache mbele ya wanahabari.

Msanii wa Muziki wa Taarabu Khadija Kopa akitoa msisitizo wa wasanii kuendelea kumuunga mkono rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutangaza yale mazuri ambayo amekuwa akiyafanya katika kusukuma kurudumu la maendeleo Tanzania.

 *Wasanii wapewa fursa adhim kutembelea mradi wa standard garge Na Khadija Seif, Globu ya Jamii. Shirika la reli nchini (TRC) limetoa nafasi kwa wasanii kutembelea mradi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge ili kujionea unavyoendelea. Mradi huo wa reli ya Kisasa ya Standard Gauge umeanzia jijini Dar es Salaam na kuelekea Morogoro utarahishisha usafiri wa abiria na mizigo, pia inatarajia kukuza biashara kati ya Tanzania na nchi Jirani kama vile Burundi, Rwanda na DRC kwa kuwa baadaye itaendelezwa kwenda hadi nchi zote zilizoko mpakani mwa Tanzania. 

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mtendaji Mkuu wa shirika la reli nchini (TRC) Jamila Mbarouk amesema ni fursa adhimu kwa wasanii pamoja na waandishi wa habari kwa pamoja kupanda treni hiyo kwa lengo la kuangalia mradi huo uliweza kujengwa kwa awamu mbali mbali. Mbarouk amesema Safari hiyo itasaidia kutangaza utalii uliopo ndani hasa kuwepo kwa treni hiyo ya umeme ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo ya tani elfu 10 huku iikiwa na spidi ya kilomita 160 kwa saa. "Shirika la reli (TRC) limewapa kipaumbele wasanii, wachoraji, wacheza mpira, Washehereshaji (MC), Waimbaji watakuwa mabalozi wazuri katika kuutangazia umma treni hiyo kukagua Standard Garge mpya itakayotoka Dar es salaam hadi Morogoro" alisema Mbarouk.

 Aidha ameeleza treni hiyo imeitengeneza kwa pesa za watanzania kutokana na kodi zilizokusanywa. Mbarouk ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi ili iweze kusaidia uchumi wa Tanzania maana bila kodi hakuna maendeleo. Kwa upande wake Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amepongeza uongozi wa Shirika la Reli (TRC) kwa kuwapa fursa wasanii na kutambua mchango wao katika jamii. "Mkuu wa mkoa Paul Makonda anakaribisha kwa wote wanaohitaji mikopo aliyohaidi wakati wa Mkutano wa wasanii wote nchini kuweza kupata mkopo huo utakaowezesha kufanya kazi kwa weledi mzuri ili kukuza tasnia zote nchini." alisema Nyerere. 

 Ameongeza kuwa ni vyema wasanii kuendelea kutangaza mema yote yanayofanywa na rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo Watanzania kwa kuwa wao ni vioo vya jamii na wananguvu kweli kuleta mabadiriko.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube