KAMANDA CHOUGHULE: VIJANA TUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE KWA KUFANYAKAZI ZA KUJIAJIRI
Friday, October 14, 2016
Sharik Chughule |
Mwenyekiti wa CCM, Shina la Pamba Road, Dar es Saaam, Sharik Choughule, amewaasa vijana kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kufanya kazi za kujiajiri.
Amesema, kufanya hivyo kutawawezesha vjana wengi kuwa na ajira za uhakika, badala ya kusubiri ajira za serikali au taasisi mbalimbali kwa kuwa nafasi za ajira katika sekta hizo ni chache huku mahitaji yakiwa ni makubwa.
Choughule ambaye pia ni Kamanda wa Vijana Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam, amesema hayo leo wakati akizungumzia kumbukumbu ya miaka 17 ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambayo Maadhimisho yake yanafayika leo Kitaifa mkoani Simiyu kwa shughuli ya kuzima Mwenge.
Amesema, ili kuweza kufanya kazi za kujiajiri, vijana ni lazima kwanza kuondoa woga, ili kujiamini kuwa wanaweza kwa kuwa ajira binafsi zipo nyingi hasa ikizingatiwa kwamba wengi siku hizi wana elimu za kutosha hadi za viwango vya Chuo Kikuu.
"Vijana lazima tujiamini kwa kuwa sisi ndiyo tegemeo la taifa, hivyo siyo busara vijana kuanza kulalamika kuwa hatuna ajira kwa lengo la kutarajia kuwa Taifa ndilo tulitegemee kutupatia ajira, hayo si mawazo mwafaka kwa afya ya nchi yetu", alisema Shoughule.
Alisema, hatua ya vijana kuanza kuweka kisingizio cha ukosefu wa ajira za kuajiriwa, kinawadumaza vijana na kukosa maamuzi ya kubuni au kukosa ubunifu wa kubuni miradi aina tofauti tofauti kwa manufaa yao.
Choughule alisema, hivi sasa umefikia wakati wa vijana kuachana na mawazo mgando, kwa wasababu baadhi ya vijana ambao wameonyesha uthubutu, wameweza kujiajiri katika sekta za mitandao ya mawasiliano ambayo ni sekta imeenea duniani kote.
Alisema, mfano mzuri wa kuigwa ni vijana walipo Jeshi la Kujenga Taifa, JKT, ambao wamekuwa wakionyesha kufanya kazi nyingi ambazo siyo za kuajiriwa ikiwemo kuanzisha shughuli za kilimo cha kisasa, ufugaji na ufundi wa aina mbalimbali ikiwemo kutengeneza samani na ujenzi wa nyumba.
Choghule amesema, hatua ya vijana kufanyakazi za kujiajiri siyo tu watakuwa wamemuenzi Baba wa taaifa Mwalimu Nyerere, lakini pia watakuwa wamemuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika azma yake ya kukuza uchumi wa taifa kwa kaulimbiu yake ya 'Hapa kazi tu'.
No comments:
Post a Comment