Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kununua kila goli kwa Sh5 milioni litakalofungwa na Simba na Yanga katika michezo yao ya kimataifa mwishoni mwa wiki hii. Ametibitisha Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.
Simba itakuwa mwenyeji wa Raja Casablanca Februari 18 mwaka huu katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikiwaalika TP Mazembe Februari 19, 2023, mechi zote zitachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.