TIMU ya taifa ya Argentina imetwaa taji la Copa America baada ya ushindi wa bao 1-0 mbele ya Brazil katika mchezo wa fainali uliochezwa usiku wa kuamkia leo.
Ni Angel Di Maria alipachika bao la ushindi dk 22 ambalo lilidumu mpaka dakika ya 90. Argentina pia ilipiga jumla ya mashuti 6 huku mawili yakilenga lango na Brazil wao walipiga 13 na mawili yalilenga lango.
Licha ya uwepo wa staa wa Brazil Neymar Jr ndani ya kikosi hicho bado alishindwa kuipa ushindi timu hiyo ambayo ilikuwa inapambana na staa wa Argentina, Lionel Messi.
Ilikuwa ni fainali ya kibabe Uwanja wa Maracana ambayo ilishuhudia jumla ya kadi 9 za njano zikitolewa ambapo Argentina wao walionyeshwa 5 na Brazil 4