BREAKING

Tuesday 31 December 2019

MKULO ASEMA HANA MPANGO WA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KILOSA, MOROGORO 2020



Na Mwandishi Wetu, Morogoro.

Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Morogoro Mustafa Mkulo (pichani) ameshangazwa na baadhi ya watu kudai anataka kugombea ubunge katika jimbo la Kilosa huku akikanusha hana mpango wowote wa kugombea nafasi hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Morogoro katika salamu za mwaka mpya wa 2020 ikiwa ni sehemu ya kawaida yake kufanya hivyo kila mwisho wa mwaka, Mkulo amesema ajabadilisha maamuzi yake ya kutogombea nafasi ya ubunge na kushangwazwa na baadhi ya watu kudai anataka kuombea tena nafasi hiyo.

“Kuna watu wamekuwa wakidai nataka kugombea tena ubunge Kilosa hizi ni habari za uongo sina mpango wa kugombea ubunge sehemu yoyote ile hapa nchini “ amesema Mkulo.

Mkulo amesema bado anajivunia katika miaka 10 ya ubunge jimbo la Kilosa kwa kutekeleza ilani ya chama kwa kipindi hicho na Wana-Kilosa kuridhika na utendaji wake.

Aidha Waziri waziri huyo mtaafu wa Fedha amesema ataendelea kuwa mwanachama na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hata hivyo amefafanua kuwa pamoja sio mbunge na wala hafikirii kugombea nafasi hiyo lakini ataendelea kutoa mawazo yake kwa CCM na hata kusaidia wasiojiweza kwa niaba ya CCM ili chama kiweze kutekeleza mipango yake ya kimaendeleo.

Katika salamu zake za mwaka 2020 Mkulo amesema anafurahishwa na utendaji kazi mzuri wa Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli na anaunga na wanaCCM wengi kutomuingilia katika katika uchaguzi wa kipindi cha pili ya miaka mitano ijayo 2020 hadi 2025 ili aweze kutekeleza kwa ufasaha mipango ya kimaendeleo alioicha katika awamu ya kwanza.

“Huu ni utaratibu wangu wa kila mwaka kutoa salaumu za mwaka mpya tangu nikiwa mbunge na sasa ni wakati wa kusema ukweli Rais Magufuri kwa miaka minne amefanya mengi mazuri anahitaji pongezi kutoka kwa Watanzania hasa katika kupandisha uchumi na kuboresha miundombinu ya nchi hii” amesema Mkulo.

Mustafa Mkulo ni Mbunge Mstaafu ambaye aliongoza kwa miaka 10 katika jimbo la Kilosa ambapo pia katika kipindi hicho alishika nafasi ya Waziri wa Fedha na kuacha kugombea mwenyewe kwa hiari yake katika uchaguzi 2015 na nafasi yake ikachukuliwa na Mbunge wa sasa Mbaraka Bawaziri ambapo amesema maamuzi yake ya kuacha kugombea ni kutoa nafasi wa wanaCCM wengine kuchangia mawazo yao katika kuliletea maendeleo jimbo la Kilosa.

TCAA WAZINDUA MFUMO WA KIDIGITALI WA KUSAIDIA KUTUA NDEGE KATIKA KIWANJA CHA NDEGE CHA MPANDA - KATAVI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania,Mizengo Pinda kwa pamoja wakikata utepe kuasharia kuuzindua mfumo wa kidigitali utakaowezesha ndege kutua salama katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi. Afisa Muongoza Ndege Mwandamizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA Sunday Walinda akimpatia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe maelezo ya kitaalamu kuhusu mfumo wa kidigitali utakaowezesha ndege kutua salama katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi. Rubani wa Shirika la ndege la Tanzania Rubani Hamza akielezea namna mfumo huo ulivyorahisisha hatua za utuaji ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda, Katavi. Viongozi walioketi meza kuu wakipungia ndege ya Shirika la ndege la Tanzania kama ishara ya kuitakia safari njema ilipokuwa ikipaa kutoka uwanja wa ndege wa Mpanda, Katavi. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari akielezea mchakato mzima ukinzia na tafiti na hatimaye kubuniwa kwa mfumo huu wa kidigitali wa kuziwezesha ndege kutua salama katika uwanja wa ndege wa Mpanda, Katavi. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe, akielezea kufurahishwa na jitihada zilizofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kufanikisha mfumo huu kukamilika sambamba na kuipongeza mamlaka hiyo kwa kutumia wataalamu wazawa waliobuni mfumo huu katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi. Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh Juma Zuberi Homera ameipongeza TCAA kwa kubuni mfumo huu na kusisitiza kuwa wananchi wa Mpanda watumie fursa hii ya ujio wa ndege mara tatu kwa wiki kujiimarisha katika kuwekeza kwani milango ya biashara na wageni zaidi kufika mpanda kwa usafiri wa anga sasa imerahisishwa. Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda akiwachagiza wanaMpanda kuitumia fursa hii ya ujio wa ndege katika wilaya hiyo kujinufaisha kiuchumi.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube