BREAKING

Monday, 25 April 2016

MUUNGANO TIMU YA BUNGE KUMENYANA NA WENZAO WA BARAZA LA UWAKILISHI ZANZIBAR

Timu ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania Bunge Sports Club inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo mkali na wa aina yake ambao ni wa kwanza na timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mapema leo Aprili 25.2016 timu hiyo ilishuka katika dimba hilo la Amani na kupasha misuli maalum kwa hiyo mchezo huo wa hiyo kesho ambapo kwa mujibu wa viongozi wa timu hiyo ya Bunge wametamba kuibuka na ushindi wa kishindo.
Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto ametamba kwa timu yake kuibuka na ushindi mnono katika mchezo huo kwani wana mazoezi ya kutosha na pia wamejiandaa kuonyesha uwezo.
“Tunawaomba wabunge wote kutuunga mkono katika mchezo huu kwani tmu imejindaa vya kutosha kuhakikisha tunashinda. Mchezo huu ni maalum kwa ajiri ya kuimalisha Muungano wetu tukufu hivyo tutaendelea kuuenzi na kuukumbatia na sote kwa pamoja tuzidishe Amani” alieleza Mh. Mwamotto.
Kwa upande wake Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani 'Maji Marefu' ambaye ni miongoni mwa viongozi wa msafara wa timu hiyo ya Bunge ametamba timu yake kuibuk na ushindi mnono kwani wamejiandaa kisaikolojia na mazoezi ya kimichezo.
Naye Mbunge wa Nzega Vijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla viongozi wa timu hiyo ya Bunge amebainisha kuwa, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya Saa 12 Jioni kesho Aprili 26.2016 katika uwanja huo wa Amani.
“Mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Utachezwa kesho ni siku ya Kuadhimisha Muungano wa Nchi ya Jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Tunawaomba watu kujitokeza kwa wingi kuuona mchezo huu ambao utakuwa wa aina yake kwa timu zote mbili.” Alieleza DK. Kigwangalla.
Timu hiyo ya Bunge yenye wachezaji Zaidi ya 19 imejiandaa vya kutosha katika kuakikisha inapata ushindi mnono na ipo Visiwani hapa kwa maandalizi ya mchezo huo tokea jana na leo imeweza kufanya mazoezi ya awali asubuhi na mengine wakitarajia kufanya hapo jioni.
DSC_1627Timu ya Bunge ikifanya mazoezi yake mapema leo Aprili 25 kuajiandaa na mchezo huo utakaochezwa keshi Jioni uwanja wa Amani.
DSC_1741Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani 'Maji Marefu' akisimamia mazoeszi hayo kwa muda wakati wsa asubuhi ya leo
DSC_1664mazoezi hayo yakiendelea..
DSC_1627Mazoezi yakiendelea
DSC_1742 DSC_1679DSC_1684Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto (kati) akitoa maelezo ya mazoezi hayo
DSC_1636DSC_1717Benchi la ufundi likiwa tayari katika mazoezi hayo
DSC_1751DSC_1721Mbunge William Ngeleja akijaribu kutaka kuchukua mpira kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla.
DSC_1683Mazoezi moto moto yakiendelea..
DSC_1687Mazoezi makali ya timu ya Wabunge yakiendelea katika uwanja wa Amaan, Unguja leo Aaprili 25.2016. Timu hiyo kesho Aprili 26 inatarajia kucheza mchezo wao dhidi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog, Zanzibar).

Friday, 22 April 2016

SHIRIKISHO VYUO VYA ELIMU YA JUU WAPONGEZA UTEUZI WA HAPPI NA, POLEPOLE KUWA MA-DC


Katibu Shirikisho Vyuo Vya Elimu ya Juu Siraji Madebe
akizungumza leo na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam
NA BASHIR NKOROMO
Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu CCM, limepongeza Uteuzi wa vijana, Salum Happi na Humphrey Polepole kuwa wakuu wa wilaya uliofanywa hivi karibuni.

Katika pongezi hizo, Katibu wa Shirikisho hilo, Siraji Madebe, amewataka Happi (Kinondoni) na Polepole (Musoma) na Vijana wengine waliopatiwa nafasi mbalimbali, kuchapa kazi kwa bidii ili wasi kuendelea kuudhihirishia umma wa Watanzania kwamba Vijana wanao uwezo wa kushika madaraka.

Amesema, ni muhimu wajitume kwa sababu kutochapa kazi kwa bidii kutasababisha Umma uonekane umefanya makosa kuwaamini vijana, jambo ambalo halitarajiwi kutokea.

Pamoja na pomgezi hizo, Katibu wa Shirikisho hilo, amezungumzia masuala mengine ikiwemo changamoto dhidi ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, zinazotokana na utendaji wa TCU na Bodi ya Mikopo. >>>IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI 

UTANGULIZI;
Ndugu wandishi wa habari,awali ya yote nipende kutanguliza shukrani za dhati kwa Mwenyezi mungu mwingi wa rehema kwa kuendelea kutupatia uzima na Afya ili kutekeleza majukumu ya kitaifa.

Lakini pia Shirikisho la Wanafuzi  Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania linampongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kuendelea kutumbua majipu na Kuadabisha wote wanaokiuka Utaratibu, sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma hasa Wezi, Mafisadi, Wala rushwa na Watendaji wazembe wa Serikali, Tunamwomba Mh Rais kutorudi nyuma wala kuhofia chochote kwani Watanzania Zaidi ya Milioni 45 tupo naye katika maombi na kumuunga Mkono kwa dhati.

USHIRIKI WA VIJANA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI
Ndugu wandishi wa habari,itakumbuka kuwa Serikali ya awamu ya nne (4) ya Mh Jakaya Mrisho Kikwete aliwateua Vijana wengi kupata fursa za Uongozi wa Nchi yetu

Katika awamu hii ya tano (5) pia chini ya MH Rais Dr John Pombe Magufuli , Ushiriki wa Vijana Umeshamiri na zaidi Tunaendelea kushuhudia wakishika nafasi Mbali mbali na tena za ngazi ya juu kabisa ikiwemo Mawaziri, Naibu Waziri, Wakuu wa wilaya na Wakuu wa Mikoa.

Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya Juu Taifa, kwa niaba ya vijana wote Tunawapongeza Vijana wenzetu wote waliopata Uteuzi katika nafasi mbali mbali

Tunatoa pongezi za kipekee kwa uteuzi wa Vijana wenzetu uliofanywa na Mh Rais kwa ndugu Salumu Happi kuwa Mkuu wa wilaya Kinondoni na Humphrey Polepole  kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma hili ni heshima na Faraja kubwa kwa kuaminiwa na Taifa na kupewa majukumu ya kumuwakilisha Mh Raisi kwa ngazi ya hiyo ya wilaya.

 Ni dhahiri bila kigugumizi uteuzi huo umeendelea kuwa ishara kuwa  serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inaimani kubwa na vijana katika kusimamia na kutekeleza majukumu kwa uaminifu na ufanisi mkubwa. Hii ikiwa ni kutokana  na uwezo na ufanisi wa hali ya juu 

ulioonyeshwa na vijana mbalimbali waliopo na waliotangulia kuwa mfano katika taifa letu.

Tunapenda kumshukuru Mhe. Rais kwa kuwa na imani na kuendelea kuwaamini vijana kumwakilisha kwenye nafasi mbalimbali za kuhakikisha mambo yanakwenda mbele.

 Nitoe mwito kwa vijana tuendelee kutunza imani hizi na uaminifu kwa viongozi bila ya kuwaangusha kwa ustawi wa maendeleo kwa Taifa letu. Mungu awaongoze kwa kila jambo na awaepushe kwa kila baya kwa ufanisi na Maendeleo ya Watanzania.


CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI
Vile vile Shirikisho la wanafunzi la vyuo vya elimu ya juu Tanzania linatumia fursa hii kuzungumzia kidogo kuhusu changamoto dhidi ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu zinazotokana na wakala wa Udahili wa wanachuo nchini (TCU) na Bodi ya Mikopo.

 Kufuatia hizo chagamoto,Shirikisho la Wanafunzi Vyuo Vya Elimu juu Taifa linaiomba serikali kupitia bodi ya mikopo na TCU kuweza kutatua changamoto zifuatazo kwa wanafunzi;-


TANZANIA UNIVERSITY COMISSION (TCU)
·        Kusajili vyuo visivyokuwa na sifa.
 Hii inapelekea wanafunzi kunyimwa haki yao ya msingi kama vile >kukosekana kwa mitaala inayokidhi haja na maadili ya somo husika, >kukosekana kwa madarasa ya kutosha kufundishia wanafunzi wote
> Kukosekana kwa wakufunzi wa kutosha na wenye sifa ya kufundisha masomo husika.
 Hata hivyo tatizo hili linapelekea kufungwa kwa vyuo hivyo mara  vinapoonekana kukosa vigezo jambo ambalo linaathiri wanafunzi katika masomo yao na hata kisaikolojia mfano St. Joseph Arusha baada ya chuo kufungwa wanafunzi waliathirika kwa kiasi kikubwa kwa sababu wengi walikuwa kwenye mpango wa five years (5) special programme ambao haukuwepo kwenye vyuo vingine.

Ombi kwa serikali
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa inaiomba Serikali kupitia bodi ya TCU ifatilie kwa kina na kuchukulia hatua vyuo vyote ambavyo havikidhi mahitaji ya wanafunzi ikiwemo na Mitaala. Pia tunaiomba bodi ijitahidi kujiridhisha kwa kina na chuo kabla ya usajili ili kuondokana na usumbufu wa kufunga chuo husika wakati wanafunzi wanaendelea na masomo

·        Kuwepo kwa tozo ya quality assurance fees.
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa, inaiomba TCU iangalie upya maana upande mwingine ni tatizo kwa wanafunzi.Hasa vyuo ambavyo vipo chini ya NACTE wanafunzi wengi wao hawana Mikopo na hata Wanafunzi Ambao wapo chini ya TCU, Tunaomba Mh Waziri wa Elimu pamoja na Bodi nzima ya TCU kukaa na kupitia Upya Hiyo tozo ili iweze kuondolewa kwa wanafunzi ambao wengi wao ni watoto wa maskini na wakulima wanaosoma kwa shida  

BODI YA MIKOPO
·        Kucheleweshwa kwa malipo ya mahitaji ya wanafunzi kama vile pesa ya chakula, malazi na special facult requirements.
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya Juu Taifa, Inasikitika kuona Bodi ya Mikopo inachelewesha  kutoa pesa za wanafunzi ndani ya muda husika na    Kushindwa kufika kwa wakati kwa pesa hizi kunapelekea migomo na uchochezi wa kukosekana kwa amani mashuleni, pia inarudisha nyuma maendeleo ya wanafunzi kwa sababu  wengi wanashindwa kumudu gharama za masomo na mahitaji ya kila siku hivyo kushindwa kuhudhuria vipindi vya darasani kabisa na hivyo kutofanya vizuri katika masomo yao.

Ombi kwa serikali
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa, inaiomba serikali kupitia bodi ya mikopo kukamilisha malipo ya wanafuzi kwa wakati ili waweze kuwa na utulivu mashuleni na waweze kupata haki yao ya msingi katika kufanikisha masomo yao.
·        Kucheleweshwa kwa ada za wanafunzi wanaodhaminiwa na bodi.
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa, inaona hii ni changamoto kubwa inayopelekea kuyumba kwa huduma zinazopaswa kutolewa na chuo kwa ajili ya kufanikisha elimu bora kwa kila mwanafunzi. Huduma kama vile kuwalipa wakufunzi, kukarabati madarasa na kununua vifaa vya kufundishia na kufanyia majaribio kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi, zinashindwa kupatikana kwa wakati na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya wanafunzi katika masomo yao. Aidha bodi inalipa ada kidogo kidogo kwa wanafunzi wake mfano; bodi inaanza kulipa million 100 kwanza wakati pesa inayohitajika ni 1bilioni

Ombi kwa serikali
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa, Tunaiomba serikali kupitia bodi ya mikopo kukamilisha malipo ya ada vyuoni kwa wakati na kuachana na malipo kidogokidogo ili kuweza kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa ufanisi mkubwa.

·        Mikopo ya misimu kwa wanafunzi.
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa, inaona  Mikopo hii inatokana na kukosekana kwa utaratibu mzuri wa muendelezo wa malipo mwanafunzi anapoanza masomo kuanzia mwaka wa kwanza hadi anapohitimu. Wapo wanaofanikiwa kupata mkopo kipindi wanapoanza masomo na kushindwa kuendelea kupata mkopo katika muendelezo wa masomo hayo. Hii ni changamoto kubwa sana hasa kwa wanafunzi wasioweza kumudu gharama za mahitaji yao pindi wanapokuwa masomoni hivyo kupelekea kurudisha nyuma maendeleo yao na wengine kushindwa kuendelea na masomo.

Ombi kwa serikali
Kama bodi inaweza kudhamini mwanafunzi kuanzia mwaka wa kwanza mpaka atakapohitimu ifanye hivyo ili kuwawezesha wanafunzi hao kumaliza masomo yao na kupata elimu bora inayowastahili.
·        Ubaguzi katika utolewaji wa mikopo kwa wanafunzi.
Bodi ya mikopo hutoa kipaumble kwa wanafunzi wa education na sayansi kuliko masomo mengine, hii ni changamoto kubwa kwa wanafunzi wasiosoma masomo hayo kwa sababu inawanyima fursa ya kupata elimu hasa kwa wale wasiokuwa na uwezo mzuri kiuchumi.
Ombi kwa serikali Utolewe ufafanuzi wa kutosha kuhusiana na jambo hili ili wanafunzi waelewe sababu zinazopelekea jambo hili kuwepo.

Siraji Shaa  Madebe
K/KATIBU MTENDAJI MKUU
SHIRIKISHO LA WANAFUNZI
WA VYUO VYA ELIMU YA JUU
                                                      04/22/2016

Tuesday, 19 April 2016

MBUNGE WA MKURANGA MH. ABDALLAH ULEGA AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI

ule1
        Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akikabidhi jezi seti 20 na mipira 20 kwa walimu
        na manahodha wa shule zote za Sekondari zilizopo wilayani humo jana .shule hizo hivi sasa
                    zipo kwenye maandalizi ya mashindano ya UMISETA Picha na David John
ule2 

MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amekabidhi jezi seti20 na mipira 20 zenye thamani ya sh.milioni 4katika shule zote za Sekondari zilizopo katika Jimboni hapa. Akikabidhi jezi hizo wilayani hapa jana katika hafla fupi iliyowakutanisha walimu wakuu,wanamichezo,watendaji wa halmashauri ,pamoja na Ofisa Elimu ,Ulega amesema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge. Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya. "Ndugu zangu walimu na manahodha wa timu zote Kutoka shule 20 za sekondari zilizoponda ndani ya Jumbo langu la Mkuranga nimetoa vifaa hivi ili muweze kushiriki vyema katika michezo ya shule za Sekondari UMISETA nakutuletea mafanikio,"alisem Ulega pia amesema kuwa anatambua kuwa kuna changamoto za kutosha katika michezo hususani vifaa vya michezo Kwa kutambua hilo ameamua kutoa vifaa hivyo huku akiwataka wanafunzi na walimu hao kusimamia vyema. Aidha Mbunge Ulega amehaidi kutoa ushirikiano wa dhati Kwa walimu na viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo ili Kwa pamoja kuharakisha maendeleo jimboni hapa ikiwamo michezo. Pia amewaambia viongozi hao kujenga mashirikiano ya Katibu na yeye kama mwakilishi wao yupo tayari Kwa wakati wowote kutumika na kusikiliza maoni yao. Kwaupande wake Ofisa Elimu wa Halmashauri Kwa upande wa shule za Sekondari Benjamini Majoya akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa Mbunge Ulega amefanya jambo ambalo halijawahi kufanywa Kwa viongozi wengine waliotangulia. Amesema kuwa watamuunga mkono Mbunge huyo Kwa kuhakikisha wanafanya vizuri katika nyanja ya Elimu na michezo Kwa ujumla. "Kwanza tunashukuru Kwa vifaa hivi kwani vimekuja katika wakati muhimu ambapo tunakwenda katika mashindano ya UMISETA na Kwa vifaa hivi ushindi upo,"amesema Majoya Pia ameongeza kuwa hakuna ubishi kwamba michezo ni ajira hivyo lazima watahakikisha vijana hao wanafanya vizuri katika michezo na taaluma pia

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AZINDUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA 2D NHC MOROGORO


Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akifunua pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la jengo la biashara na Ofisi la 2D la mjini Morogoro lililojengwa kwa thamani ya Shilingi bilioni 4.3. Jengo hilo ni la ghorofa nne likiwa na eneo la chijni kwa ajili ya maegesho ya magari . Ni mradi wa kwanza kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu mara tuu baada ya kuwashwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa akiupokea kwenge mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.
Meneja wa Shirika la Taifa, Veneranda Seif akiupokea kwenge mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.
Meneja wa Shirika la Taifa, Veneranda Seif akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.
Jengo la Biashara la 2D linavyoonekana leo kabla ya kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya.
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa akijiandaa kuupokea Mwenge wa Uhuru.
Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo wakijiandaa kuupokea Mwenge wa Uhuru.
Mwenge wa Uhuru ukiwasili katika eneo la tukio.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Issack Peter akiupokea Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika eneo mradi wa 2D.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo ambapo alilipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha wanawapatia wananchi makazi bora na akalitaka Shirika kuendeleza jitihada hizo ili Watanzania wengi zsaidi wafaidike.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo ambapo alilipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha wanawapatia wananchi makazi bora na akalitaka Shirika kuendeleza jitihada hizo ili Watanzania wengi zaidi wafaidike.
Wafanyakazi wa Ashirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo ambapo alilipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha wanawapatia wananchi makazi bora na akalitaka Shirika kuendeleza jitihada hizo ili Watanzania wengi zaidi wafaidike.

MULTICHOICE TANZANIA WATANGAZA WASHINDI WA "JISHINDIE NA DSTV

bmn2.0-620x308Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akizungumza kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu ya droo hiyo pamoja na ofa mbalimbali zinazoendelea kutolewa kwa wateja wa DSTV
DSC_1452Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo akichanganya droo hiyo kwa njia ya kielektoniki kupitia kompyuta. wengine wanaoshuhudia ni maafisa wa MultiChoice Tanzania. Kulia ni mwakilishi kutoka Bahati Nasibu ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Millao.
DSC_1453Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akihakiki moja ya majina ambayo yameingia kwenye droo ya ushindi kwa wateja wa DSTV
DSC_1463Droo hiyo ikiendelea
DSC_1451Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionyesha majina ya washindi kwenye 'sreen' kubwa (Haipo pichani) wakati wa tukio hilo
DSC_1484Droo hiyo ya JISHINDIE NA DSTV ikienndelea huku maafisa wa MultiChoice Tanzania na Mwakilishi wa Mchezo wa kubahatisha Tanzania pamoja na wanahabari wakishuhudia tukio hilo mapema leo Aprili 19.2016, Makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya MultiChoice Tanzania inayosambaza vifaa vya ving’amuzi vya DSTV hapa nchini mapema leo Aprili 19.2016 imechezesha droo maalum na kuwapata washindi wa “JISHINDIE NA DSTV” katika tukio lililofanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbay, barabara ya Ali Hasan Mwinyi, Jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.
Awali katika droo hiyo, Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo alieleza kuwa, droo hiyo ilianza tokea mwezi wa kwanza ambapo wateja walitakiwa kuwa na malipo kwenye ving’amuzi vyao vya DSTV bila kukatika kuanzia hiyo Januari hadi mwezi Machi.
Wateja ambao hawajakatiwa ving’amuzi vyao katika promosheni hiyo ya JISHINDIE NA DSTV, waliotangazwa leo ambaoo ni wateja waliojiunga mwezi wa kwanza na kuweza kulipia DSTV zao bila kukatiwa matangazo kwa muda wa miezi mitatu wameweza kujishindia zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar wakiwa wao na familia zao.
“Washindi wawili ambao kila mmoja atapata nafasi ya kupelekwa Zanzibar na kukaa huko kwa siku mbili katika hoteli huku akilipiwa kila kitu kuanzia usafiri, malazi, chakula yeye na familia yake ikiwemo baba, mama na watoto wawili. Washini hao ni Mwelly Nyakusaima ambaye ni mkazi wa Igoma-Mwanza na mshindi mwingine ni Evarist Ndambo mkazi wa Tabataa Jijini Dar es Salaam.” Alisema Bi. Hilda Nakajumo.
Aidha, alibainisha kuwa, washindi wengine waliojishindia droo hiyo ambao ni wa kipengele cha pili ni wale wateja ambao tayari walishajiunga na DSTV huku wakitakiwa wasikatiwe malipo yao kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa tatu.
Ambapo wateja 50 wamejishindia DSTV EXPLORA Decoders huku wateja 90 wao wakibahatika kupata kuunganishwa malipo ya bure ya mwezi ikiwemo ya mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita na miezi 12 bure.
Aidha, washindi hao wote walioshinda MultiChoice ilibainisha kuwa, watapigiwa simu na kuelekezwa namna ya kuchukua zawadi zao hizo kuanzia sasa kwa muda hadi June mwaka huu.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu aliwakumbusha wateja wa DSTV kuendelea kulipia malipo ya ving’amuzi vyao huku wakitoa ofa mbalimbali sambamba na vipindi vizuri ikiwemo vya uhondo wa soka la kimataifa, filamu na muziki..





Wednesday, 13 April 2016

UJUMBE WA MAWAZIRI NA WAFANYABIASHARA WA CZECH REPUBLIC WAFANYA KONGAMANO LA UWEKEZAJI DAR ES SALAAM

 2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Misitu wa Serikali ya Czech Republic Bw. Dusan Benza akizungumza katika kongamano la wafanyabiashara wa nchi hiyo na watanzania lililofanyika leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Mawaziri wawili Kilimo na Viwanda wa Jamhuri ya Jamhuri ya Czech wakiongozana na wafanyabiashara zaidi ya thelathini wako nchini kwa ajili ya kutafuta na kujionea fursa za uwekezaji nchini Tanzaniam Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na Tanzania Investiment Bank (TIB), Ubalozi wa Szech Republic nchini Kenya na Tanzania House Of Business Company Limited (THB).
Ujumbe huo metembelea wizara ya Kilimo na wizara ya Viwanda na Biashara na kusaini mikataba ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hapa nchini na nchi ya Szech Republic ili kuunganisha masuala ya kibiasha na uwekezaji na kuwezesha wafanyabiashara wa nchi hizi kuwekeza katika masuala ya biashara, Teknolojia na Kilimo kwa ujumla.

Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic hapa nchini John Chaggama akizungumza na mmoja wa viongozi wa ujumbe huo huku Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa Czech akisikiliz kwa makini.
4
Injinia Michal Basovnik wa kampuni ya Impuls akitoa mada kuhusu shughuli mbalimbali zinazotolewa na kampuni yao ambayo ina tawi pia nchini Zambia.
5 7
Injinia Martin Adamuska wa kampuni ya NWT kutoka nchini Czech Republic akifafanua jambo wakati alipokuwa akielezea mambo mbalimbali yanayofanya na kampuni yao lakini pia fursa mbalimbali zinazoweza kuwekezwa.
8
Injinia Petr Pawlica wa wa kampuni ya PAWLICA pia ametoa mada katika kongamano hilo na kuelezea teknolojia ya kampuni hiyo katika masuala ya Kilimo. 9
Bw. Godffrey Kirenga wa SAGCOT CENTER LIMITED akiwaelezea wafanya biashara hao juu ya fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini katika uwekezaji wa kilimo.
10
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza katika kongamano hilo kulia ni John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania.
11 12
Kutoka kulia ni Mr Charles Chandika Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania House Of Business Company Limited, Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate nchini Tanzania, Elipina Makungu na Bahija Salim wakijadiliana jambo wakati wa kongamano hilo la wafanya biashara.
13
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza na Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate nchini Tanzania wakimsikiliza mmoja wa maofisa kutoka wizara ya mambo ya nje wakati akizungumza nao.
14
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye na John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania wakizungumza na Injinia Vladmir Pikora wa benki ya Czech Export Bank mara baada ya nusu ya kwanza ya majadiliano kati ya wafanya biashara wa Tanzania na Szech Republic katika kongamano lililofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
15
John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ujio wa wafanyabiashara hao.
16
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa ujio wa wafanyabiashara hao na kongamano hilo kwa wafanyabiashara wa Tanzania ya Czech Republic katika masuala mazima ya kibiashara na uwekezaji.
17
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini Czech Republic wakiwa katika kongamano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
18 19
Baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania wakihudhuria kongamano hilo.
20
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali za Tanzania masuala ya biashara na uwekezaji wakiwa katika kongamano hilo.
21
John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania akimsikiliza Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate nchini Tanzania.
22
Elipina Makungu na Bahija Salim wakifurahia jambo wakati wa kongamano hilo la wafanyabiashara wa Czech Republic na Tanzania kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube