BREAKING

Saturday, 16 January 2021

DSTV YAMWAGA OFA KWA WATEJA WAKE YATAJA PROMOSHENI KABAMBE YA 'PANDA TUKUPANDISHE'



MultiChoice Tanzania imetangaza promosheni maalum kwa wateja wa DStv ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu itakuwa ikiwapandisha vifurushi wateja wake. 


Hii ni promosheni inayowawezesha wateja wa DStv wanaokidhi vigezo (wateja waliokatika, wateja wanaoendelea na wateja wapya) kupata fursa ya kulipia kifurushi kinachofuatia cha juu yake na kupandishwa kwa kupatiwa kifurushi cha juu ya kile walicholipia kwa muda maalum.  Hii itategemea na kifurushi ambacho mteja alikuwa amelipia hadi kufikia tarehe 8 Januari 2021 au kifurushi alichojiunga nacho baada ya tarehe 8, Janurai 2021. Mathalan, 

Mteja wa kifurushi cha Bomba, akilipia kifurushi cha Family, atapandishwa hadi kifurushi cha Compact bila malipo ya ziada kwa mwezi mmoja.


“MultiChoice Tanzania inafurahi kuzindua rasmi promosheni yake maalum ya ‘Panda tukupandishe’ hii ikiwa ni njia mojawapo ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kuwa nasi na pia njia ya kuwahakikishia kuwa tumejipanga vema kuendelea kuwapatia burudani isiyo na kifani” amesema Ronald Shelukindo, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania wakati wa uzinduzi rasmi wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam.


Amesema kampuni hiyo inaendelea kuwapatia wateja wake burudani ya kina bila kusahau maudhui mengine kama Habari na elimu, huku ikihakikisha kuwa wateja wake wanapata maudhui kemkem na ya kusisimua ya ndani na nje.  

Kaimu meneja wa thamani kwa wateja Lucy Kisasa amesema kama zilivyo promosheni nyingine, kuna vigezo na masharti ambavyo vitafuatwa ili mteja aweze kunufaika na promosheni hii. Amesema promosheni hii ni kwa wateja wa DStv waliopo Tanzania, wale ambao akaunti zao ziko hai na wale ambao akaunti zao zimekatika. Pia inawahusu wateja wapya wa DStv wanaojiunga sasa na huduma hizo. 

Amesema mteja wa DStv anayelipia kifurushi cha juu ya kile anachotumia au cha mwisho kutumia atapandishwa kifurushi kwa muda wa mwezi mmoja bila malipo ya ziada na pia mteja mpya wa DStv aliyejiunga siku ya, au baada ya tarehe 8 Januari 2021 ambaye atalipia kifurushi cha juu ya kile alichojiunga nacho naye pia atanufaika na ofa hii. 

Hata hivyo, wateja wa DStv ambao wamelipia kifurushi chao kwa mwaka mzima hawahusiki na promosheni hii kwani hawa tayari wana ofa yao ambapo hupata mwezi mmoja wa kifurushi chao bila malipo ya ziada.  


Amefafanua kwamba Mteja atakayetaka kulipia kifurushi cha juu yake kabla kifurushi alichonacho hakijaisha naye atanufaika na ofa hii na pia salio lake la kifurushi cha awali litaendelea kubaki kwenye akaunti yake na hivyo kuwaza kulitumia tena punde ofa aliyopata itakapokamilika kulingana na vigezo na masharti.

Wednesday, 13 January 2021

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE -KULA CHAKULA NA WATOTO YATIMA UKUMBI WA KIBADA GARDEN -KIGAMBONI MUFTI WA TANZANIA ALI KIBA , KUJUMUIKA...







 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete anatarajiwa kushiriki chakula cha Mchana na watoto yatima wa kituo cha Amani Foundation For ORPHANAGES -Kigamboni January 16 mwaka huu.. 

Wageni wengine ambao wanatarajiwa kushiriki katika Chakula cha Mchana katika tukio ambalo litaambatana na uchangiaji Uimarishaji wa Kituo hicho ni pamoja na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeiry Ally, Sheikh Mkuu wa Mkoa Alhad Mussa Salum  ,Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.Faustine Ndugulile  sambamba na Mwanamuziki wa kizazi kipya Ali Kiba....

Thursday, 7 January 2021

LAMECKY NYAMBAYA KIONGOZI MPOLE USONI! MWENYE HAIBA YA UANA MICHEZO...MUUMINI WA SOKA LA VIJANA.




Na Said makala

Nelson Mandela, rais wa kwanza wa Afrika Kusini kuchaguliwa kidemokrasia na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, , alifariki Desemba 5, mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 95, Mandela aliwahi kutumikia kifungo kwa miaka 27 kwa sababu ya mapambano yake dhidi ya mfumo wa kibaguzi wa Afrika Kusini unaofahamika kama  Ukaburu, Aliachiwa huru kutoka gerezani mwaka 1990, na kuwa rais miaka minne baadae, na kuachia madaraka baada ya kutumikia kwa kipindi kimoja tu, kitendo adimu kufanywa na wenye madaraka barani Afrika.

Ni Mpambanaji aliyeonyesha uwezo wa kuongoza kwa vitendo, yes! alikuwa mtu mhimu sana katika Ulimwengu wa siasa , wacha nisiseme ya kisiasa hapa nataka kumzungumzia mtu mmoja anaitwa Lamecky Nyambaya Mwenyekiti Mpya wa Chama cha soka Mkoa wa Dar es Salaam, mtu jasiri hususani kuhamasisha soka nchini ambaye alianza kujiimarisha kwenye uongozi wa soka la Vijana 

Mwaka Jana Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) siku ya Jumapili,ya  Novemba 29,mwaka  2020 Ulifanyika uchaguzi na kupata viongozi wapya ambao wataongoza  chama hicho kwa miaka minne, nafasi hiyo ya Mwenyekiti iliyokuwa imeachwa wazi na Almasi Kasongo ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi (TPLB) tayari ina mtu sahihi mwenye haiba ya aina yake mtu mwenye moyo wa kusaidia soka popote anapokwenda, Huyoni Lamecky Nyambaya...


 Lameck Nyambaya aliyekuwa mgombea pekee na kupata kura 27 aliaminiwa zaidi na hiyo inatokana na utendaji wake wa kazi uliotukuka akiwa Mjumbe wa soka ndani ya Shirikisho la soka tanzania TFF,  akiwakilisha Mkoa wa Dar es salaam , hivi sasa bila shaka kupewa mikoba ya kuwa Mwenyekiti DRFA mengi mazuri yanakuja , katika mwaka wa 2021 Nyambaya anatakiwa kuzingatia mambo mengi lakini machache nitayataja na ni haya yafuatayo ili haiba yake iweze kutimia zaidi na kuendelea kupata sifa za kiongozi...

Kwanza.. .Nyambaya anapaswa kuendeleza pale Almas Kasongo alipoachia na kupiga mbizi ndefu kuleta maendeleo ya soka kwa kuwa tayari ana uzoezfu wa kuongoza, 

Pili.. .Azungumze na wadau kupata kilio cha wanamichezo kwani wapo wazazi ambao wanaaminiu kuwa vijana wao kudidimia katika soka ni kupoteza mwekeo sawa na wale wanaoingia katika shindano la Miss Tanzania wakiamini kule ni kujidhalilisha bila kujua kuwa huko kuna vipaji vinavyokufa kutokana na imani hizo potofu, hivyo anapaswa kuwa mshawishi zaidi kwa wazazi kupata vipaji.

Tatu...Nyambaya asijifungie Ofisni asiwe na Umangi Meza hayo yote akiepuka tunamuona Nyambaya mkubwa katika uendelezaji wa soka Tanzania kwa miaka ijayo

Hizo ni nguzo chache ambazo zinanishawishi kuamini Lamecky Nyambaya ni mtu mwenye malengo ya haki na maamuzi ya busara kila mara anapoamua kusaidia soka, naamini amekuwa karibu na familia ya soka amekuwa mwenye huruma na familia ya soka kama alivyo na huruma kwa familia yake hivyo wadau washikamane naye katika kuhakikisha soka linakuwa zaidi kwani yupo katika jiko bora la Dar es salaam, ambalo limejaa viungo vya kila aina , nikimanisha Mkoa wa Dar es salaam, ndio wenye vipaji vya kila aina....mimi nashawishika kumwita Lamecky Nyambaya ni Kiongozi wa mfano kwa kuwa hana Mbwembwe anatekeleza mambo yake kwa vitendo.


WAZIRI MWIGULU APONGEZA UONGOZI WA MAHAKAMA KWA KUTOA USHIRIKIANO NA KUWAPA NGUVU TAWJA KUFANIKISHA KAZI ZAO


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo wakati akimuwakilisha akimuwakilisha Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza. (Picha Zote Na Mathias Canal)

Mgeni rasmi-Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akikabidhiwa Tuzo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake (TAWJA) Mhe Jaji Joaquuine De-Mello kwa kutambua mchango wake kwa majaji na mahakimu wanawake mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe Prof. Ibrahim Hamis Juma akikabidhiwa Tuzo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake (TAWJA) Mhe Jaji Joaquuine De-Mello ya kutambua mchango wake kwa Majaji na Mahakimu wananwake wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Geofrey Pinda akisisitiza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake (TAWJA) Mhe Jaji Joaquuine De-Mello akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.

Na Mathias Canal, Wizara ya Katiba na Sheria-Mwanza


Serikali imefurahishwa kwa kazi zinazofanywa na Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake TAWJA katika kupigania haki za wananchi.


Hayo yamebainishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akimuwakilisha Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.


Amewataka majaji hao kuendelea kuongeza na kuimarisha Haki za Wanawake katika suala la Haki Sawa kwa wote; Kukuza Upatikanaji wa Haki kwa Wanawake, Kukuza/Kuendeleza Uongozi wa Mahakama; Kufanya tafiti za kisheria katika Usawa wa Kijinsia na Haki za Binadamu; Kubadilishana taarifa katika masuala tata yanayowahusu Wanawake na kuondoa Upendeleo wa Kijinsia na Ubaguzi wa aina yeyote.


Amesema kuwa mtazamo mkubwa wa TAWJA ni kuhakikisha Majaji Wanawake na Mahakimu pamoja na Maafisa wengine wa Mahakama na Washirika wanaandaliwa kwa kuwapatia nyenzo sahihi na muhimu zinazohitajika katika kukuza Haki Sawa kwa Wote (‘Equal Justice for All’)


Ninafahamu kuwa mmekuwa mkifanya hivyo bila kuchoka kwa kipindi cha miaka ishirini (20) mfululizo tokea TAWJA kuanzishwa kwake mwaka 2000. Kwa hili niwapongeze sana Wanachama wote, mnatakiwa kujivunia na kutembea kifua mbele kwa kazi nzuri mnazofanya. Naamini kuwa hili lisingewezekana bila msaada mkubwa kutoka kwa Mahakama ya Tanzania Bara na Zanzibar” Alikaririwa Dkt Mwigulu


Dkt Mwigulu amesema ni wazi kuwa sauti zao Majaji na Mahakimu Wanawake ikijumuisha na zile za Wadau wengine nchini zimepelekea utayari, uwazi na hamasa katika kulaani ubaguzi na ukiukwaji wa Haki za Binadamu unaofanywa na wanajamii katika maeneo yetu.


Waziri Mwigulu amesem akuwa kaulimbiu ya Mkutano huo ni; “Weledi na Ustawi wa Majaji Na Mahakimu Wanawake: Chachu ya Mabadiliko”, imekuja wakati muafaka na mahali sahihi kwani mara nyingi Wanawake Wataalamu hawatilii maanani ustawi wao, na hasa Maafisa wa Mahakama ambao muda wote hutingwa zaidi na majukumu yao ya msingi.

 

Kutokana na Kaulimbiu hiyo, mtaibua vitu vingine vilivyojificha na vinayowakabili Maafisa wa Mahakama amesisitiza katika mkutano huo kujadiliwa kwa kina kuhusu masuala yahusuyo afya za akili na mwili na kudadavua kuhusu uchumi, masuala ya kisaikolojia sambamba na kuangalia ukuaji katika maeneo ya utoaji haki.


“Maendeleo ya Mwanamke ni maendeleo ya wote. Hivyo ni lazima kumpa mwanamke kipa umbele. Ni muhimu sana kumpa mwanamke nafasi nyingi bila kujali kuwa ni haki yake ya msingi kwani pia ni kuonyesha matumizi mazuri ya uelewa wa uchumi.” Amesisitiza

MAISHA MAGIC BONGO YAZIDISHA UHONDO WA BURUDANI TAMTHILIYA MPYA ZA JUA KALI NA PAZIA ZA BAMBA KINOMA

Mambo ni bandika - bandua, paukwa – pakawa ndani ya chaneli maarufu ya Maisha Magic Bongo (MMB) ambapo imetangaza rasmi kuanza kwa tamthilia mbili kabambe za Pazia na Jua Kali, zitakazoanza kurushwa kuanzia Januari 2021 kwenye Chaneli ya MMB DStv 160.

 

Kiu ya mashabiki wa tamthilia za kibongo imepata dawa kwani tamthilia mpya ya Pazia imepikwa ikapikika huku ikisimamiwa na mzalishaji maarufu na kijana mtanzania Samwel Isike, ambaye pia ndiye aliyezalisha tamthilia iliyojizolea umaarufu mkubwa hapa nchini ya Sarafu.

 

Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akimtambulisha mzalishaji mkuu wa tamthilia mpya ya PAZIA Samwel Isike wakati wa uzinduzi rasmi wa tamthilia mpya za kitanzania za PAZIA na JUA KALI zinazorushwa katika chaneli ya Maisha Magic Bongo – DStv 160.

 

 

Tamthilia hii imeaanza kurushwa kuanzia January 4, 2021 na inaonekana Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 Jioni. Tamthilia hii imejaa mikasa, visa, vitimbi bila kusahau mafunzo yatokanayo na maudhui yake. Tamthilia hii imesheheni vinara wa uigizaji hapa nchini akiwemo Jacqueline Wolper anayeigiza kama Miriam Lewa bila kumsahau Hisani Muya anayeigiza kama Henry Lewa

 

Wasanii wanaoigiza katika tamthilia mpya ya PAZIA wakijitambulisha mbele ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa tamthilia mpya za kitanzania za PAZIA na JUA KALI zinazorushwa katika chaneli ya Maisha Magic Bongo – DStv 160. Miongoni mwa waigizaji hao ni (kutoka kulia) Tino Muya  (Henry), Welu Sengo (Eliza), Ben Pol (Ben) Nasma Hassan (Regina) na Akim Juma (Edu).

 

 

Uhondo hauishii hapo, kwani mzigo mwingine unaoshushwa ndani ya MMB ni tamthilia ya Jua Kali kutoka kwa mzalishaji maarufu mwanadada Leah Mwendamseke, ambaye mbali ya kuwa ni mzalishaji wa tamthilia maarufu ya Kapuni pia ni mshindi wa tuzo mbalimbali katika tasnia ya filamu.

 

Wasanii wanaoigiza katika tamthilia mpya ya JUA KALI wakijitambulisha mbele ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa tamthilia mpya za kitanzania za PAZIA na JUA KALI zinazorushwa katika chaneli ya Maisha Magic Bongo – DStv 160. Miongoni mwa waigizaji hao ni - kutoka kushoto - Romy Jones (Bill Junior) Abbot Charles (Frank) Leah Mwendamseke na  Wansukula Zacharia (Tuma).

 

Tamthilia hii ya Jua Kali itaanza kutingisha jiji mnamo Januari 6, 2021 na itakuwa ikirushwa saa 3.30 usiku Jumatano hadi Ijumaa. Huku nako kuna waigizaji nguli kama  Rainfredd Masako anayeigiza kama Professor Bili na kumejaa vituko na mikasa ya kila aina ambapo wapenzi wa tamthilia hawatapenda kuikosa au kusubiri kusimuliwa.

 

Mtangazaji maarufu nchini Rainfred Masako ambaye anaigiza kama Profesa Bill katika tamthilia mpya ya JUA KALI akiwasalimu washiriki wa hafla ya uzinduzi rasmi wa tamthilia mpya za kitanzania za PAZIA na JUA KALI zinazorushwa katika chaneli ya Maisha Magic Bongo – DStv 160. Hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za DStv Tanzania ilihudhuriwa pia na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo. 

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamthilia hizo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo, amesema kuwa serikali inathamini na kutambua mchango mkubwa wa MultiChoice katika kukuza na kuendeleza tasnia ya filamu hapa nchini. Amesema kitendo cha chaneli ya Maisha Magic Bongo kuwa na maudhui mengi ya ndani kimekuwa ni chachu ya ajira nyingi katika tasnia lakini pia kimeongeza ushindani na ubora wa kazi za wazalishaji wetu.

 

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo akizungumza wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa tamthilia mpya za kitanzania za PAZIA na JUA KALI zinazorushwa katika chaneli ya Maisha Magic Bongo – DStv 160. Hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za DStv Tanzania ilihudhuriwa pia nawasanii na waigizaji wa tamthilia hizo na waandishi wa habari.

 

Dr. Kiagho amesema kuwa yeye binafsi amekuwa akiwatemebelea wasanii na kujionea uzalishaji wa filamu mbalimbali hapa nchini na ameridhishwa na kuongezeka kwa ubora na weledi katika uzalishaji wa filamu na maudhui mengine. Amewataka wasanii kutumia fursa hii vizuri na kuhakikisha kuwa wanaongeza ubora wa kazi zao ili ziweze kushindana katika soko la ndani na nje na hivyo tasnia ya filamu kuongeza mchango wake katika uchumi wa wasanii na taifa kwa ujumla

 

 

 

Naye Mkuu Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo, amesema mbali na kutumia wasanii na waigizaji wakongwe, wamehakikisha kuwa kuna mchanganyiko na waigizaji wapya na vijana ambao wanaleta vionjo vipya na vya kisasa katika tamthilia hizo na hivyo kuzifanya kuwa kivutio kikubwa kwa watazamaji wa rika zote.

“Kila mara tunaleta maudhui kulingana na matakwa ya wateja wetu, tunhakikisha kuwa tunawapatia maudhui yaliyoboreshwa na yenye vionjo vipya kila uchao bila kusahau uhalisia wa kitanzania kwenye maudhui yetu” alisema Ronald na kuongeza kuwa wanafurahi sana kufanya kazi na wazalishaji na waigizaji wa Tanzania na hivyo kuzidi kukuza vipaji vya wasainii wetu na kuwapa ulingo wa kuonyesha umahiri wao katika fani.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo (wa pili kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo wakati wa uzinduzi rasmi wa tamthilia mpya za kitanzania za PAZIA na JUA KALI zinazorushwa katika chaneli ya Maisha Magic Bongo – DStv 160. Hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za DStv Tanzania ilihudhuriwa pia nawasanii na waigizaji wa tamthilia hizo.

 

Amesema kuwa katika miaka 5 tangu chaneli hiyo ianzishwe, mamia ya wazalishaji na wasanii wa Tanzania wamepata fursa ya kuuza kazi zao na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza soko la maudhui hususan filamu hapa nchini.

Saturday, 19 December 2020

AZAM FC YA MSEMAJI ZAKA ZA KAZI NA ILE YA LWANDAMINA INAVYOSHANGAZA....

 


Nelson Mandela, rais wa kwanza wa Afrika Kusini alikuwa wakwanza kuchaguliwa kidemokrasia na hatimaye akaja kuwa Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, ,alifariki 
Desemba 5,mwaka  2013 akiwa na umri wa miaka 95, alikuwa shujaa kila wakati alizungumza kwa staha , alisema maneno kwa adabu na hekima , mafano aliwahi kusema  "I am not a saint, unless you think of a saint as a sinner who keeps on trying.”  akiwa na maana kuwa " Msinihukumu kwa mafanikio yangu, nihukumuni kwa mara ngapi nilianguka na kuinuka tena"Mwisho wa kunukuu, sina maana ya kuzungumza siasa hapa ninachotaka kukizungumza ni kimoja katika soka husuani Msemaji wa Azam FC Zaka za Kazi Vs Lwandamina.... Zaka ni Msemaji hodari, lakini Lwandamina ni Kocha Mahiri wa Azam FC vitendo vya Lwandamina na Zaka ni Mbingu na Ardhi wakati Zaka akituaminisha msimu huu ubingwa unatua ndani ya klabu hiyo kocha wao Mzambia akili yake wala haimsikilizi kwani hadi sasa Azam FC sare zao ni mfanano wa Maua jana Azam FC ilikubali sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Desemba 18, Uwanja wa Azam Complex, ukiwa ni mwendelezo wa matokeo mabovu kwa Lambalamba hao

Katika mchezo wa jana nyota njema ilianzia kwa Nyota wa Azam FC Ayub  Lyanga alikuwa wa kwanza kucheka na nyavu dakika ya 34, bao hilo lilidumu mpaka muda wa mapumziko na kuwafanya vijana wa Charles Mkwasa kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa nyuma kwa bao moja.

 Kipindi cha pili Iliwachukua dakika 7 Ruvu kuweka mzani sawa kupitia kwa Emmanuel Martin baada ya kipindi kuanza kwa kufunga bao dakika ya 53 ambalo lilidumu kwa muda wa dakika 7 likapinduliwa na Mudahthiri Yahya dakika ya 60.


Ruvu walitumia dakika 10 kusawazisha bao hilo ambapo dakika ya 70 Fully Zully Maganga aliweka mzani sawa na kufanya ubao usome 2-2.

Ni Idd Seleman kwa Azam FC alionyeshwa kadi ya njano huku wajeda wanne walionyeshwa kadi za njano kutokana na nguvu na spidi ndani ya Uwanja wa Azam Complex.


Hii inakuwa ni sare ya pili mfululizo kwa Azam FC ndani ya Uwanja wa Azam Complex baada ya mchezo wao uliopita kufanya hivyo mbele ya Namungo FC na iligawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 2-2.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ibaki nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 16 kibindoni ina pointi 29 huku Ruvu ikiwa nafasi ya nne na pointi 25 nayo pia imecheza michezo 16.


DORTUMUND YAOKOTWA JALALANI TENA,MOUKOKO AWEKA REKODI YAKE

Mshambuliaji kinda wa Klabu ya Borussia Dortmund, Youssoufa Muokoko  usiku wa kuamkia leo amefunga bao la kwanza ndani ya Ligi ya Uingereza maarufu kama Bundesliga na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo kufunga kwenye ligi hiyo.

Nyota huyo mwenye miaka 16 amevunja rekodi ya nyota wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz ambaye alifunga akiwa na miaka 17 ilikuwa dhidi ya Bayern Munich akiwa  Mei 2020.

Dortmund ambayo ilimchimbisha kocha wao Lucien Favre wiki iliyopita baada ya kupokea kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya VfB Stuttgard nafasi iliyochukuliwa na Edin Terzic ilifungwa mabao 2-1 dhidi ya Union Berlin na Moukoko alifunga bao lake la kwanza.

Nyota huyo mzaliwa wa Cameroon amesema kuwa ni furaha kubwa kwake kufunga kwenye mchezo huo ilikuwa dakika ya 60 licha ya timu yake kupoteza jambo ambalo litawafanya wapambane kwa ajili ya mechi zao zijazo.

Mabao ya wapinzani wao yalipachikwa na Taiwo Awonyi dakika ya 57 na lile la ushindi lilipachikwa dakika ya 78 na Marvin Friedrich alipachika bao la ushindi na kuifanya Union Berlin kusepa na pointi tatu mazima Uwanja wa Alle Forsterel.

Matokeo hayo yanaifanya Dortmund iwe nafasi ya nne na pointi 22 baada ya kucheza mechi 13 Bayer Leverkusen  ni vinara wakiwa na pointi 28.



 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube