BREAKING

Monday, 23 May 2016

ENGLAND YAITANDIKA UTURUKI

Timu ya soka ya Taifa ya England imeanza maandalizi ya fainali za Mataifa ya Ulaya, 2016 kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Uturuki.
Ushindi huo ulipatikana katika katika Mechi ya kirafiki iliyopigwa katika Uwanja wa Etihad Jijini Manchester kupitia wachezaji Harry Kane anayeichezea Tottenham na Jamie Vardy wa Leicester City.
England walifunga Bao lao Dakika ya 3 kupitia Harry Kane na Turkey kusawazisha Dakika ya 13 kwa Bao la Hakan Calhanoglu.
Kipindi cha Pili Dakika ya 71 England walipata Penati baada ya Jamie Vardy kuangushwa na Topal lakini Harry Kane alikosa Penati hiyo kwa kupiga nje.
Dakika ya 83 Jamie Vardy aliipa England Bao lao la pili kufuatia Kona ambapo Gary Cahill alipiga Kichwa Golini na Kipa wa Turkey Babacan kugongana na Beki wake na kutoa mwanya kwa Vardy kufunga.
Katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa Marekani imefanikiwa kuichapa Puerto Rico mabao 3-1.

BARCELONA YATWAA KOMBE LA MFALME...



Klabu ya soka ya Barcelona imefanikiwa imetwaa kombe la Mfalme Hispania, maarufu kama Copa del Rey katika Fainali ya 114.

Wachezaji nyota Jordi Abba na Neymar ndio walio iwezesha Barcelona kutwaa taji hilo katika Fainali iliyopigwa Jijini Madrid kwenye Uwanja wa Atletico Madrid wa Estadio Vicente Calderon.

Hii sasa ni  Fainali ya 37 ya kombe la kwa Barcelona huku Barca wakishinda mara ya 28 sasa, kombe hilo pia  Barca walitwaa Kombe hilo kwa kuifunga Athletic Bilbao 3-1.

TRA YAWAPA ELIMU YA MLIPAKODI WAFANYABIASHARA RAIA WA CHINA WAISHIO NCHINI TANZANIA

1Meneja wa Elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA Bi. Diana Masalla akitoa elimu ya mlipa kodi na sheria za kodi kwa wafanyabiashara raia wa China wanaoishi hapa nchini na kufanya biashara katika semina ya mlipa kodi iliyofanyika leo kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam, ambapo kabla semina hiyo imefunguliwa na Bw. Sun Chengfeng Mwakilishi wa masuala ya Kiuchumi na Kibiashara kutoka serikali ya Watu wa China nchini Tanzania, Semina hiyo inalenga kuwapa wafanyabiashara hao elimu na uelewa wa masuala mbalimbali ya kisheria katika kodi na umuhimu wa kulipa kodi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE)
2 3Baadhi ya wafanyabiashara raia wa China wanaoishi nchini Tanzania na kufanya biashara wakiwa katika semina ya mlipa kodi iliyofanyika leo kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam
4Bw. Sun Chengfeng Mwakilishi wa masuala ya Kiuchumi na Kibashara kutoka Serikali ya Watu wa China nchini Tanzania akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina hiyo iliyofanyika kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam.

Thursday, 12 May 2016

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA RAJABU LUHWAVI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA CCM MKOA WA PWANI LEO


 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Rajab Luhwavi akivishwa Skafu na Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Omari Salum, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, Wilayani Kibaha mkoani humo leo.  Katikati ni Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga na kulia ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Kibaha,  David Malecela.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rajab Luhwaavi, akiongozana na  Katibu wa CCM mkoa wa Pwani, Joyce Masunga, kwenda Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, wilayani Kibaha leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwai akisalimia baada ya viongoi baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, kuzungmza na wafanyakazi wa CCM mkoa wa Pwani wilayani Kibaha leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwai akisalimia baada ya viongoi baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, kuzungmza na wafanyakazi wa CCM mkoa wa Pwani wilayani Kibaha leo 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwavi akisaibi kitabu cha wagei katika Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, wilayani Kibaha leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Pwani, Joyce Masunga.
 Watumishi wa CCM wakimkaribisha ukumbini Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rajab Luhwavi akiingia ukumbini kuzungumza na wafanyakazi wa CCM wilaya za mkoa wa Pwani katika kikao alichofanya na wafanyakazi hao katika Ofisi ya CCM ya mkoa iliyopo wilayani Kibaha.
 Naibu Katibu Mkuu Luhwai baada ya kuwasili ukumbini
 Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga akisoma taarifa 
 Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga akisoma taarifa

HIF LINDI YAWAPA ELIMU YA TOTO AFYA KADI AKINA MAMA WA HALMASHAURI YA (W) LIWALE

1Meneja wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi akitoa elimu ya mpango mpya na wa gharama nafuu utakaomuwezesha mzazi kumlipia bima ya Afya mtoto chini ya miaka 18 unaojulikana TOTO AFYA KADI,kwenye kliniki ya mama na mtoto (RCH) Hospitali ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
2 
Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Liwale akitoa rai kwa akina mama walioudhuria kliniki kwa kuchangamkia fursa kwani ni mpango wenye manufaa zaidi na una uwigo wa mafao kwa 50,400 tu.
3 
Akina mama wakifuatilia elimu ya kitita cha mafao yanayotolewa kwenye mpango wa Toto afya kadi kutoka kwa meneja wa NHIF Lindi hayupo pichani.

Thursday, 5 May 2016

SNURA AKUBALI YAISHE,AJITETEA KUFUNGIWA WIMBO WAKE..

Mwimbaji wa nyimbo za Mduara nchini Snura Mushi ameomba radhi kwa umma wa Watanzania kwa kosa la kutengeneza, kuzindua na kuweka mitandaoni, video ambayo imefungiwa jana na Serikali kupitia Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na Michezo kutokana na ukiukwaji wa maadili ndani ya wimbo huo na video yake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Jijini Dar es Salaam Snura ameomba radhi kwa mashabiki wake na watanzania wote akisema wakati wa utayarishaji wa video hiyo hakutambua kama ingepokewa tofauti, hivyo atafanya jitihada za kuhakikisha anauboresha zaidi.

Naye meneja wake alizungumzia utetezi huo akiomba watanzania kuwasamehe yeye pamoja na msanii huyo, kwani sasa wamejifunza ikiwepo kupata usajili wa BASATA utakaomwezesha kufanya kazi zake kwa huru.

TIMU YA MENEJIMENTI YA NHC NCHI NZIMA YATEMBELEA MIRADI YA SHIRIKA HILO JIJINI DAR ES SALAAM.

1Meneja Mradi wa Shirika l nyumba la Taifa NHC Kawe unaokwenda kwa jina la 711 Injinia Samwel Metil akitoa maelezo kwa Timu ya Menejimenti ya NHC wote(Directors, Regional Managers & Line Managers) wakati walipotembelea miradi ya 711 Kawe , Morocco Square, Victoria Place, Eco Residence na Kibada ambapo ambapo pia watafanya pia kazi katiia miradi hiyo Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kuwafahamisha juu ya maendeleo na changamoto za miradi hiyo.
2
Mmoja wa Mainjinia wa Mradi wa 711 Kawe Bw.Kishor Hirani akimelezea jambo Meneja mradi Injinia Samwel Metil wakati menejimenti ya shirika hilo ilipotembelea katika mradi huo.
3
Wakuu wa vitengo mbalimbali na mameneja wa mikoa wakitembelea mradi wa 711 Kawe leo.
4
Mmoja wa Mameneja wa NHC kutoka mkoani Dodoma Bw. Itandula Gambalagi pamoja na wenzake wakiwasili kutembelea mradi wa Morocco Square.
5 6Wakipatiwa maelezo katika mradi wa Morocco SquareMorocco Square
7Mameneja hao wakifuatilia maelezo ya mradi wa Morocco Square
8
Muungano Saguya kulia Yahya Charahani kushoti na Itandula Gambalagi wakijadiliana jambo wakati walipotembelea mradi wa 711 Kawe pamoja na wenzao.
9
Jengo la Mradi wa Eco Residents ambalo limekamilika kwa asilimia 99%.
11Ujenzi wa mradi wa 711 Kawe ukiendelea.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube