BREAKING

Friday, 21 February 2025

UPANDIKIZAJI WA MENO BANDIA KWA NJIA YA KISASA MUHIMBILI MLOGANZILA 45 KUNUFAIKA NA HUDUMA








Katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita  za kuboresha huduma za afya nchini  Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imenza kambi maalum ya upasuaji wa upandikizaji wa meno bandia kwa njia ya kisasa kwa wagonjwa ambao wamepoteza meno yao kutokana na sababu mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kambi hiyo Daktari Bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno MNH.Mloganzila Dkt. Peter Shempemba  amesema wagonjwa watakao hudumiwa katika kambi hiyo ni pamoja na wale ambao walifanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwaka jana na wale ambao wanakuja  kwa mara ya kwanza.

Ameongeza kuwa kundi la kwanza ni wale  ambao walishawapandikiza mizizi ya meno katika awamu ya kwanza na kipindi hiki watapandikizwa meno na kundi lingine  ni wale ambao wanapandikizwa mizizi kwa mara ya kwanza.

“Upandikizaji huu ni wa ubora wa hali ya juu, meno tunayoyapandikiza hayana tofauti na meno ya asili kwakuwa yanapandikizwa moja kwa moja kwenye mfupa wa taya na yanadumu kwa   muda mrefu, hayawezi kutoka kirahisi, mtu ataweza kutafuna vizuri kama kawaida ” amesema Dkt. Shempemba.

Kambi hiyo inafanyika kwa kushirikiana wataalam wa ndani na Daktari Bingwa aliyebobea katika Upasuaji wa Taya kutoka Hospitali za Wochhardt Dkt. Chirag Desai ambapo itafanyika kwa kipindiki hiki cha siku saba kuanzia tarehe 20 hadi 26 Februari, 2025 ambapo takribani wagonjwa 45 watafanyiwa upandikizaji.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube