BREAKING

Friday, 10 January 2025

DCEA YAFANIKIWA OPERESHENI DAWA ZA KULEVYA YAKAMATA JAHAZI DAWA ZA KULEVYA




Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeeleza kuridhishwa na oparesheni zilizofanyika mwaka jana 2024 kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola ambapo ilifanikiwa kukamata dawa za kulevya Kilogramu 673.2 za Methamphetamine na heroin, miongoni mwa hizo, kilogram 448.3 ziliwahusisha raia wanane wa Pakistani.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo amesema sehemu kubwa ya dawa hizo zikikamatwa katika bahari ya Hindi katika harakati za kuingizwa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema Serikali ya awamu ya sita kuputia mamlaka ya kudhibiti Dawa za Kulevya DCEA kwa mwaka 2024 ilifanya mapinduzi makubwa katika kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya na kwamba katika dawa zilizokamatwa zipo zilizokutwa zimefichwa ndani ya jahazi la raia hao wa Pakistan.

Aidha katika hatua nyingine Kamishna huyo amesema Serikali inaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha inaikinga jamii dhidi ya Madhara yatokanayo na dawa za kulevya akieleza pia jinsi watumiaji wanavyotumia vibaya bahari ya Hindi kufikisha madawa hayo nchini.

NAIBU WAZIRI MKUU AKARIPIA UZEMBE TANESCO



 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko amekerwa na utendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akitoa maagizo uongozi wa kituo cha miito ya simu (call centre) ufumuliwe.


Maagizo ya Dk Biteko kwa Tenesco ni kufuatia kutotekelezwa kwa maagizo yake ya aliyoyatoa mwaka jana ya kuwepo kwa namba ya mawasiliano ya wateja isiyolipiwa ambapo itamwezesha mteja kupiga simu bila kukatwa salio  agizo ambalo halijatekelezwa.

Dkt Biteko ameyatoa maagizo hayo  baada ya kutembelea kituo cha miito ya simu Tanesco ambapo amesema watendaji wa shirika hilo wamezoea kazi.



 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube