BREAKING

Friday, 10 May 2019

WAZIRI BITEKO AZINDUA SOKO KUU LA MADINI MWANZA

Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefanya uzinduzi wa Soko Kuu la Madini Mwanza na kutumia fursa hiyo kuwahimiza wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kutumia soko hilo kuuzia madini yao na kuachana na tabia ya utoroshaji wa madini.

Uzinduzi wa soko hilo unganishi Kanda ya Ziwa umefanyika Mei 08, 2019 katika jengo la Rock City Mall ambapo Biteko amebainisha kwamba uanzishwaji wa masoko ya madini nchini umesaidia ongezeko la kiwango cha uuzaji madini tofauti na hapo awali ambapo yalikuwa yakiuzwa kiholela na hivyo kuikosesha Serikali mapato.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akitoa salamu za tume kwenye uzinduzi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akitoa taarifa ya hali ya uanzishwaji masoko ya madini nchini ambapo amebainisha kwamba zaidi ya mikoa 10 tayari imeanzisha masoko hayo.
Mfanyabiashara wa madini, Kakono Kaniki akitoa salamu kwa niaba ya wafanyabiashara wa madini mkoani Mwanza.

Mongella ajivunia Soko Kuu la Madini Mwanza "tunataka nchi ifaidike"

DC KASESELA: MARUFUKU KUFANYA BIASHARA IRINGA KAMA HULIPI KODI AU HUNA KITAMBULISHO CHA MACHINGA

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizunguza na wafanyabiashara wa bidha za kusindika walikuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali
 Wafanyabiashara wa bidha za kusindika wakiwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali na wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa bidhaa za kusindika

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Wafanyabiashara wa wilaya ya Iringa wametakiwa kufanya biashara wakiwa wamelipa kodi au wanatakiwa kuwa na kitambulisho cha wafanyabishara wadogo wadogo maarufu kama kitambulisho cha machinga.

Akizungumza na wajasiliamali waliokuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema ni marufuku kwa sasa kufanya biashara yoyote wilaya ya Iringa bila kulipa kodi na zile ambazo hazijafikia hatua kodi zitalipa tozo

“Sasa tunaanza kufanya mchakato wa kuchunguza kujua wafanyabiashara wangapi wanafanya kazi hizo bila kulipa kodi na tutawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyosema” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wafanyabiashara wadogowadogo wote wa wilaya ya Iringa kuhakikisha wanapata kitambulisho cha kwa shilling elfu ishirini ambacho kinatamruhusu kufanya biashara sehemu yoyote hapa nchini kwa mujibu wa Rais

“Jamani ili ufanye biashara kwa uhuru katika wilaya ya Iringa ni lazima uwe na kitambusho cha wafanyabisahara wadogo au uwe umelipia leseni kutoka katika mamlaka husika la sivyo huwezi kufanya biashara hiyo wilaya ya Iringa” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wananchi wote wanaopenda kufanya biashara kuhakikisha wanafanyabiashara kwa kufuata taratibu zilizowekwa na nchi ili wasipate usumbufu wowote ule kutoka kwa mamlaka za wilaya ya Iringa.

“Jamani wananchi wa Iringa changamkieni kuchukua vitambulisho vya wafanyabishara wadogo wadogo ili kufanya biashara zenu mkiwa na uhuru wa kutosha ila mkikahidi mkono wa sheria utawahusu” alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwashauri wafanyabishara ya bidhaa za kusindika kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kufuata kanuni za kisheria kwa kuhakikisha wanalipa kodi kama inavyostahili.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo walimuadi mkuu wa wilaya hiyo kuwa watahamasishana kuhakikisha wote wanakuwa na vitambulisho hivyo ili wafanye biashara kwa uhuru na haki.

“Mkuu tunakuhakikishia kuwa tutafanyabiashara huku tukiwa tumevaa vitambulisho hivi kwa kuwa Rais wetu katupa uhuru wa kufanya biashara zetu mahali popote pale bora mradi tuwe na vitambulisho hivyo” walisema wafanyabiashara hao

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube